Back to top

Waziri Hasunga awaambia wakulima 'kula maisha' kwa kutembelea vivutio

17 October 2018
Share

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe.Japhet Hasunga amewashauri Wakulima wajenge utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini mara baada ya kumaliza shughuli zao za mavuno badala ya kudhani kuwa wao ni watu wa mashambani pekee na hivyo hawastahili "kula maisha."
 
"Tengeni muda wa kula maisha, nendeni pale Hifadhi ya Taifa ya Mikumi,nendeni kule Kondoa kwenye michoro ya miambani na kwingineko mkampuzishe akili ili mkirudi mnakuwa na ari mpya.
 
Pia amewataka Wakulima hao mara baada ya kuvuna na kuuza mazao yao watenge muda wa kupumzika kwa kutembelea maeneo tofauti na yale waliyoyazoea badala ya kukaa sehemu moja pekee hali itakayowasaidia kujifunza vitu tofauti na kukutana na watu tofauti hali itakayopelekea  kupata mawazo mapya yatakayowasaidia kuongeza tija katika uzalishaji wao.