Back to top

Waziri Kalemani  aitaka bodi mpya ya REA kwenda kutatua migogoro.

16 February 2019
Share

Waziri wa Nishati Mhe Dakta Medard Kalemani amesema kuwa wakala wa umeme vijijini (REA) umekuwa na migogoro mingi isiyoisha na hivyo kuitaka bodi mpya ya wakurugenzi chini ya Mwenyekiti wake mpya Dakta Michael Nyagoga aliyeteuliwa hivi karibuni na rais ienda kutatua na kukomesha migogoro hiyo ambayo imekuwa ni chanzo cha wakala hao kutofanya kazi kwa ufanisi.

Akizungumza jijini Dodoma na wajumbe wa bodi mpya ya REA Dakta Kalemani amewataka wajumbe hao wakasimamia majukumu ya REA kwa kufuata sheria na dira ya serikali ya kufikisha umeme katika vijiji vyote nchi nzima pamoja na kusimamia fedha za miradi ipasavyo.

Aidha amezitaja baadhi ya sababu zilizopelekea bodi ya awali kuvunjwa ni pamoja na kutotekeleza majukumuyake ipasavyo na kutoyasimamia vizuri majukumu hayo jambo ambalo ameitaka bodi mpya yasijirudie.