Back to top

Waziri Mhe.Ummy Mwalimu awataka vijana vyuo vikuu kuweka mbele maslahi

20 May 2018
Share

Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mhe.Ummy Mwalimu amewataka vijana katika Vyuo Vikuu nchini kuweka mbele maslahi ya taifa na uzalendo katika kulitumikia taifa kwa maslahi ya wote badala ya kukosoa kila jambo.

Ameyasema hayo alipokwenda kuzindua Programu inayolenga kuwaongezea maarifa vijana wa vyuo vikuu nchini kujitambua na kutumia fursa zinazopatikana kujiwekea mazingira ya kujiajiri kupitia mradi wa programu ya UNI Life Kampasi alipokuwa akizungumza na  wanafunzi wa chuo kikuu Ardhi Jijini Dar es Salaam.