Back to top

Waziri Mkuu agiza kukamatwa watumishi wliotafuna bilioni tatu Geita

29 November 2018
Share

Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa ameagiza watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyangw'ale Mkoani Geita waliohusika na ubadhilifu wa zaidi ya sh. bilioni tatu fedha ambazo zilitolewa na Serikali kugharamia miradi ya maendeleo wachukuliwe hatua.

Waziri Mkuu Majaliwa pia ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa Mkaguzi wa Ndani wa halmashauri hiyo, Gavana Matesa kwa kushindwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuhusu wizi wa fedha za maendeleo zilizotafunwa.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Nyangw'ale akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Geita.

Miongoni mwa miradi ambayo fedha zake zimepotea ni pamoja na sh. bilioni 1.2 za ujenzi ofisi ya halmashauri hiyo, sh. milioni 400 za ukarabati wa kituo cha afya Nyangw'ale, sh. milioni 611.230 za miradi ya maji.

Nyingine ni sh. milioni 536.119 za mpango wa malipo kulingana na huduma (EP4R), sh. milioni 125.914 za ushuru wa huduma, sh. milioni 31 za ujenzi wa ofisi ya mbunge na sh. milioni 109 za mfuko wa barabara.
................