Back to top

Waziri Mkuu aiagiza MSD kupeleka vifaa tiba kwa wakati.

20 September 2018
Share

Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa ameitaka Bohari kuu ya dawa nchini  kuhakikisha wanapeleka vifaa tiba haraka na kwa wakati katika maeneo ambayo tayari wamepokea fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa hivyo na bado hawajapeleka huku akitoa tahadhari kwa watendaji wanaofanya ubadhirifu katika fedha zilizotengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba.

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa amesema hayo katika ziara yake  ya siku moja wilayani Kondoa mkoani Dodoma, kukagua miradi mbali ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo, ambapo akiwa katika kituo cha afya mauno ambapo amesema ni dhamira ya serikali kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wananchi wote ambapo ameitaka MSD kusimamia suala la dawa na vifaa tiba vinawafikia wananchi kwa wakati.