Back to top

Waziri mkuu akutana na Rais wa Misri.

10 July 2019
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana  na rais wa Misri Abdel Fattah Al- Sisi na kuzungumza masuala mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii na pia kuimarisha uahirikiano  baina ya nchi za Tanzania na Misri.

Mazungumzo baina ya Waziri Mkuu na Rais wa Misri yamefanyika leo Ikulu jiji Cairo, ikiwa ni katika siku ya tatu na ya mwisho ya ziara yake ya kikazi nchini Misri.

Akiwa ziarani nchini Misri, Waziri Mkuu alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly katika siku yake ya kwanza ya ziara yake, ambapo aliwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Misri waje kuwekeza nchini.

Pia, Waziri Mkuu alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo nchini humo ambayo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa makao makuu mapya ya nchi hiyo, mradi wa awamu ya pili ya upanuzi wa mfereji wa Suez Canal na kiwanda kikubwa cha ngozi.