Back to top

Waziri Mkuu atangaza mwisho wa maombolezo ya msiba wa Hayati Magufuli.

07 April 2021
Share

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa ametangaza rasmi kuwa leo ndio siku ya mwisho ya maombolezo ya aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dakta John Pombe Magufuli huku akivishukuru vyombo vya habari kwa kazi kubwa ya kuhabarisha waliyoifanya toka Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan atangaze msiba huo mkubwa.

Akizungumza jijini Dodoma na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Dodoma Waziri Mkuu amechukua nafasi hiyo kuyashukuru makundi mbalimbali wakiwemo watanzania kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha maombolezo.

Wakati huo huo Mhe Majaliwa ametoa rai kwa Watanzania kuendelea kuwa na mshikamano na umoja na kuwataka wachape kazi na kumuunga mkono Rais Mhe Samia ili Tanzania isongembele.