Back to top

Waziri mkuu atoa mwaka kwa mikoa isiyokamilisha mwongozo wa uwezeshaji

15 June 2019
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa mwaka mmoja kwa viongozi wa mikoa ya Dar-es-salaam, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa, Singida na Shinyanga ihakikishe iwe imekamilisha kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji.

Ametoa maagizo hayo  wakati akifungua Kongamano la Nne la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, kongamano hilo limeandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ambapo amewataka viongozi wa mikoa na halmashauri zote nchini wahakikishe wanaanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi kama kile cha Kahama.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuliagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuratibu mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwemo ya Serikali na ile ya binafsi ili kujua ipo mingapi na inamnufaisha nani na je wanufaika wanajijua na ni kweli wananufaika na kisha wampelekee taarifa.

Waziri Mkuu amesema mikoa yote iliyokamilisha kuandaa mwongozo wa uwekezaji, nayo ifikapo mwakani inapaswa kuonesha hatua za utekelezaji katika kutumia fursa mbalimbali zilizoainishwa pamoja na mikakati ya kutangaza fursa hizo zilizopo katika maeneo yao.