Back to top

Waziri mkuu awataka viongozi wa wilaya ya Kyerwa wajipime

10 October 2018
Share

Waziri Mkuu Mh. kassim Majaliwa amemuagiza  Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kagera Bw. Adam Ntogha kumsimamisha kazi Afisa wa Forodha katika mpaka wa Mulongo Mkoani Kagera   Bw. Peter Mtei kwa tuhuma za kujihusisha na biashara za magendo.

Akiwa katika kikao cha majumuisho na viongozi wa mkoa huo waziri mkuu Majaliwa akawataka viongozi wa Wilaya ya Kyerwa  kujipima baada ya  vitendo vya bishara ya magendo kushamiri  wilayani humo.
   
"Biashara za magendo zinafanyika bila ya wao kuchukua hatua, mnatia aibu yaani hakuna kazi inayofanyika. Viongozi wa wilaya ya Kyerwa mjipime wenyewe, mialo mingi katika wilaya yenu inatumika kwa biashara ya magendo na butura."anasema waziri mkuu Mh.Majaliwa