Back to top

WAZIRI MKUU HAJARIDHISHWA NA UJENZI HOSPITALI YA WILAYA NAMTUMBO

19 October 2022
Share

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo na kusema Serikali haiwezi kukaa kimya wakati  baadhi ya watumishi wakifanya vitendo vya hovyo.

Waziri Mkuu ametoa onyo hilo OKTOBA 18, 2022, alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Migelegele baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo, Mkoani Ruvuma.

Mapema akikagua ujenzi wa hospitali hiyo, Waziri Mkuu alikuta baadhi ya milango imepishana urefu licha ya kuwa inapaswa ikutane ili kitasa kifunge na milango mingine ilikuwa inagoma kufunga.

Waziri Mkuu amesema haridhishwi na kazi iliyofanywa kwenye hospitali hiyo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya  Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.David Silinde amesema Serikali, imeamua kujenga shule za wasichana katika mikoa yote 26 na iliyopo katika Halmashauri ya Namtumbo ni miongoni wa shule 10 za kwanza nchini ambazo zimepatiwa fedha mwaka huu.