Back to top

Waziri Mkuu kuongoza maziko ya Mwili mwingine wa ajali ya moto.

12 August 2019
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo ataongoza tena mazishi ya mwili mwingine wa ajali ya lori la mafuta katika makaburi ya Kolla baada ya miili 60 kuzikwa jana, ambapo mwili mwingine mmoja utazikwa jioni.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Stephen amesema hayo nje ya chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambapo miili miwili itasafirishwa kwenda Sengerema na Songea na itakayobaki itasubiri utambuzi na maamuzi ya ndugu.

Hali za majeruhi wote 59 wakiwemo 43 walioko Muhimbili na 16 walioko hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro wanaendelea vizuri, Kwa Mujibu wa Dk Stephen Kebwe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.