Back to top

Waziri Mkuu Majaliwa aridhishwa na mradi wa umeme wa Julius Nyerere.

10 April 2021
Share

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere katika mto Fufiji.

Amesema hayo wakati wa ziara yake katika eneo la ujenzi kujionea kazi inavyoendelea ukiwemo ujenzi wa kingo za kuzuia maji na eneo la kuchepusha maji.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutawezesha upatikanaji wa uhakika wa umeme kwa gharama nafuu ikilinganishwa na vyanzo vingine vya umeme yakiwemo mafuta na gesi ambavyo gharama zake ni kubwa mara dufu.

Aidha, amejione ujenzi wa daraja la kudumu litakalokuwa la pili kwa ukubwa, baada ya lile la Mkapa na eneo la kupokea umeme ili kuupeleka Chalinze na kusambazwa kwenda Dodoma, Kinyerezi na maeneo mengine nchini kupitia Gridi ya Taifa.