Back to top

Waziri Mkuu wa Tunisia Elyes Fakhfakh ajiuzulu.

16 July 2020
Share


Waziri Mkuu wa Tunisia Bwana Elyes Fakhfakh ametangaza kujiuzulu, tangazo lililosababisha nchi hiyo kukumbwa na mgogoro mwingine wa kisiasa.

Bwana Fakhfakh amekabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Kais Saied wa nchi hiyo, miezi mitano tu baada ya kuunda serikali mpya ya Tunisia, baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Septemba 2019.

Vyanzo vya habari vimesema Rais Saeid amemuomba Fakhfakh ajiuzulu, wakati huu ambapo Bunge la nchi hiyo lilikuwa kwenye mjadala wa kumtaka Waziri Mkuu huyo aachie ngazi, kwa tuhuma za ufisadi na utumiaji mbaya wa mamlaka.

Bwana Fakhfakh amekanusha kuhusika na masuala ya ufisadi, lakini kwa majuma kadhaa amekuwepo chini ya shinikizo kutoka kwa wapinzani waliomtaka ajiuzulu.