Back to top

Waziri Mpango aialika EU kuwekeza Tanzania.

25 February 2020
Share

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango ameuomba Umoja wa Ulaya (EU) kuwekeza katika maeneo ya maendeleo ambayo tayari Serikali imeanza kuyatekeleza ikiwemo uboreshaji wa miundombinu katika mkataba mpya wa ushirikiano kati ya Tanzania na EU kwa mwaka 2021 hadi 2027.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma wakati Waziri Dokta Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti, kuhusu ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi.

Dokta Mpango amesem katika mkataba mpya wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na umoja wa ulaya unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka 2021 hivyo ni vema ukaendelea kuimarisha maeneo ya maendeleo ambayo tayari yameanza kutekelezwa na Serikali hususani katika Sekta ya Elimu, Afya, miundombinu na mingine ili kufikia malengo endelevu.

Kwa upande wake Balozi wa EU nchini Tanzania, Mhe.Manfredo Fanti, ameipongeza Serikali kwa kuwa na Sera nzuri za maendeleo na kuboresha mazingira ya kibiashara, miongoni mwa mambo yanayohitajika ni pamoja na Miundombinu, mafunzo, kuwa na uchumi wa kidigitali na siasa bora, mambo ambayo Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuyatekeleza.