Back to top

Waziri Mpina aliomba radhi Bunge.

20 June 2018
Share

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Luhaga Mpina ameliomba Bunge radhi  kwa kutokufuata utaratibu  juu ya Maafisa wa Wizara yake kuingia katika mgahawa wa Bunge na kupima samaki waliokwishaandaliwa bila idhini ya Bunge.

Katika taarifa yake kwa Bunge Waziri Mpina  amekiri kuwaagiza maafisa kufanya ukaguzi mgahawani baada ya kugundua baadhi ya samaki waliopo katika mgahawa huo wamevuliwa chini ya viwango ukaguzi ambao ulifanyika june 19 na kusema suala hilo halikufanyika kwa lengo la kulidharau Bunge bali Maafisa wake kutokujua taratibu zinazotakiwa kufuatwa.

Akizungumza baada ya kutolewa taarifa hiyo Spika wa Bunge Mh Job Ndugai amesema Bunge limesikitishwa na kilichotokea ni kwamba linapotokea jambo lisilo sawa bungeni ni lazima bunge kupewa taarifa kabla ya kuchukua hatua kwani hata ukaguzi wenyewe haukuzingatia suala la usafi.

Baada ya kusema hayo Spika wa bunge ametangaza Bunge kusamehe na wabunge wameendelea na majadiliano ya bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19.