Back to top

Waziri wa Kilimo Mh.Japhet Hasunga atua Lindi kuhakiki Korosho.

13 November 2018
Share

Ikiwa ni siku moja tu mara baada ya kuapishwa kuongoza Wizara ya Kilimo, Waziri mwenye dhamana na Kilimo Mh.Japhet  Hasunga leo ameongoza viongozi wakuu wa Wizara yake kutembelea katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kwa ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu.

Katika msafara huo Waziri Hasunga atatembelea Mkoani Mtwara ambapo ameambatana na Naibu Waziri wa kilimo Mhe.Innocent  Bashungwa na Katibu Mkuu Mhandisi Mathew Mtigumwe watakaotembelea Mkoa wa Lindi, na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Prof Siza Tumbo atakayetembelea Mkoa wa Ruvuma.

Katika ziara hiyo viongozi hao wakuu watahakiki usimamizi wa maghala ambao kwa sasa unasimamiwa na Bodi ya usimamizi wa stakabadhi ya ghala na Usimamizi wa ziada wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko.

Vilevile watahakiki taarifa za Ubora wa maghala kama zilivyopitishwa na Bodi ya usimamizi wa Stakabadhi ya ghala  pamoja na Ubora wa ghala.

Watahakiki uwezo wa maghala na kiasi kilichopo ghalani, na kuhakikisha taarifa ya umiliki wa Korosho zilizopo kwenye ghala.

Aidha, viongozi hao watahakiki kiasi cha Korosho kwenye ghala kwa kupitia nyaraka za mapokezi ya Korosho kwenye ghala ambazo zinawasilishwa na Vyama vya msingi (AMCOS) na kuoanisha taarifa hizo na taarifa zilizomo kwenye taarifa za stakabadhi ya ghala