Back to top

Waziri wa Nishati apiga marufuku kuagiza vibarua nje ya eneo la mradi

18 September 2018
Share

Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani amepiga marufuku Mkandarasi wa kampuni ya NIPO inayotekeleza mradi wa umeme vijijini ( REA ) awamu ya tatu mzunguko wa kwanza, katika vijiji 84 vya wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza kutumia vibarua kutoka nje ya eneo la mradi huo.

Huku  akisema kazi ya kubeba nguzo za umeme hakuhitaji mtu kuwa na elimu ya shahada bali utaratibu huo unachangia kuongeza ajira kwa vijana na kuwafanya kuwa walinzi wa miradi ya umeme nchini dhidi ya watu wenye nia ya kuhujuma miundombinu ya nishati hiyo.

Waziri Dk.Kalemani ametoa agizo hilo katika kijiji cha Sanga kata ya Fukalo wilayani Kwimba mara baada ya kuzindua mradi wa umeme wa REA, ambapo zaidi ya kaya 50 zilizounganishiwa umeme huo kwenye kijiji hicho zimeanza kuonja matunda ya mradi huo.

Waziri Kalemani pia amempa rungu Mkuu wa wilaya hiyo Senyi Ngaga kuchukua hatua kali dhidi ya Meneja wa TANESCO wilayani humo pamoja na mkandarasi wa mradi huo endapo watashindwa kuwaunganishia umeme wateja waliolipia huduma hiyo kwa zaidi ya siku saba.