Back to top

Waziri wa Uganda ataka sekta binafsi kupewa nafasi.

16 June 2018
Share

                                                   Picha na Maktaba

Waziri wa Kilimo Mifugo Uvuvi na Viwanda wa Uganda Mhe. Vincent Bamulangaki Ssempijja amezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhakikisha zinashirikisha ipasavyo sekta binafsi katika mpango wa maendeleo ya sekta ya kilimo ili uweze kuajiri vinaja wengi na kwamba bila sekta binafsi mikakati ya sekta ya kilimo haitafikia malengo yaliyokusudiwa.

Mhe. Vincent Bamulangaki Ssempijja ametoa kauli hiyo katika kikao cha watalaam wa kilimo na sekta zingine kutoka nchi za Afrika Mashariki wanaokutana mkoani Arusha kujadili mbinu bora za kuboresha kilimo katika nchi za Afrika Mashariki na mchango wa kilimo katika kutoa ajira kwa vijana wa nchi hizo.

Mwakilishi mkazi wa shirika la chakula la umoja wa Mataifa FAO katika umoja wa Afrika EU David Phiri amesema kwa takwimu za mwaka elfu mbili na kumi zinaonesha zaidi ya asilimia sabini ya wakazi wa Afrika Mashariki ni vijana na hakuna sekta inayoweza kuajiri vijana wengu kama hao zaidi ya kilimo.

Mwakilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka idara ya maendeleo ya jamii Chiristopher Bazivamo amesema Jumuiya ya afrika Mashariki imeweka nguvu kubwa kwenye sekta ya kilimo kwakuwa inatambua umuhimu wake kwa vijana na maendeleo ya nchi hizo.