Back to top

WHO -Corona kutumbukiza mamilioni ya watu kwenye umasikini.

17 October 2020
Share

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana António Guterres amesema janga la Corona au (COVID-19) litawatumbukiza mamilioni ya watu katika umasikini.

Amesema katika ujumbe wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza umasikini kuwa COVID-19 ni janga juu ya janga kwa watu maskini duniani kutokana na sababu kuu mbili.

Amezitaja sababu hizo kuwa ni watu maskini kuwa hatari kubwa ya kupata virusi hivyo na pili makadirio ya hivi karibuni yanaonesha  kuwa janga la COVID-19 linaweza kuwasukumua hadi watu milioni mia moja kumi na tano kutumbukia kwenye umasikini mwaka huu.

Amesema hizi ni nyakati ngumu ambazo zinahitaji juhudi za hali ya juu kupambana na umasikini na janga la COVID-19 linahitaji juhudi imara za pamoja kulikabili.