Back to top

WHO - haina ukakika dawa Hydroxychloroquine inatibu Corona.

26 May 2020
Share

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema majaribio yanayofanyiwa dawa ya ugonjwa wa malaria Hydroxychloroquine ili kuona iwapo inaweza kutibu virusi vya Corona yamesitishwa kutokana na hofu ya usalama wake.

Vipimo vilivyokuwa vikifanywa katika mataifa kadhaa vimesitishwa kwa muda kama hatua ya kuchukua tahadhari, Hatua hiyo inajiri baada ya utafiti wa tiba uliofanyika hivi karibuni kusema kwamba dawa hiyo inaweza kuongeza hatari ya mgonjwa kufariki kutokana na virusi hivyo.

Wakati WHO ikisitisha dawa hiyo, Rais wa Marekani Donald Trump yeye amesema kuwa anatumia dawa hiyo kuzuia virusi hivyo.

Rais huyu wa Marekani ameipigia chapuo dawa hiyo ya malaria, kinyume na ushauri wa kimatibabu na onyo kutoka kwa maafisa wa Afya kwamba inaweza kusababisha tatizo la moyo.

Kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins vifo vilivyotokana na corona vimefikia 98,218.

Wiki iliopita, utafiti uliofanywa na jarida la tiba duniani Lancet ulibaini kwamba hakuna faida yoyote kwa kutumia dawa ya Hydroxychloroquine na kwamba matumizi yake yanaweza kuongeza idadi ya vifo miongoni mwa wagonjwa hospitalini walio na maambukizi ya Corona.

Inaelezwa Hydrochloroquine ni dawa salama ya kutibu ugonjwa wa malaria, baridi yabisi na Lupus, lakini hakuna majaribio yoyote ambayo yamependekeza matumizi yake kutibu Covid-19.