Back to top

WHO imesema watu laki mbili na elfu 7 wamefariki kwa ugonjwa wa surua.

14 November 2020
Share

Shirika la Afya Duniani limesema watu laki mbili na elfu saba walifariki dunia kwa ugonjwa wa surua mwaka 2019 barani Afrika,  kutokana na kukosa chanjo ya maradhi hayo, huku nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Madagascar zikiongoza.

Taarifa ya shirika hilo imesema idadi ya vifo mwaka huo ilikuwa asilimia hamsini zaidi ya kiwango cha chini zaidi cha mwaka 2016 na katika kanda zote za Shirika la Afya Duniani na idadi ya wagonjwa iliongezeka na kuwa wagonjwa laki nane, elfu sitini na tisa, mia saba sabini duniani kote.

Taarifa hiyo imesema mwaka huu kumekuwepo na idadi ndogo ya wagonjwa, lakini janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 linarudisha nyuma mafanikio katika utoaji chanjo.

Kwa sasa utoaji wa chanjo ya surua, umekwama duniani kote kwa zaidi ya muongo mmoja na kiwango cha utoaji ni kati ya asilimia 84 na 85.