Back to top

WHO yasikitishwa wataalam wake kuzuiwa kuingia China kutafiti Corona.

06 January 2021
Share

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeelezea kusikitishwa kwake baada ya timu ya wataalam wa kimataifa kukataliwa kuingia nchini China.

Shirika hilo limefanya mipango ya kutuma timu ya uchunguzi nchini China juma hili, ili kutafiti vyanzo vya virusi vya Corona na kilichotokea katika hatua za mapema za mlipuko huo nchini humo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Dkt.Tedros Adhanom amewaambia waandishi wa habari kuwa wajumbe wawili wa timu hiyo walikuwa tayari wameanza safari kuelekea nchini China, lakini maofisa wa China hawakutoa vibali vinavyohitajika kwa wao kuingia nchini humo.

Amesema aliwaomba maofisa hao wa China wahakikishe timu hiyo inaingia nchini humo bila vikwazo ili kazi iliyowapeleka ianze haraka iwezekanavyo.