Back to top

Wilaya ya Mbinga yakumbwa na uhaba wa petroli.

22 July 2020
Share

Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imekumbwa na uhaba wa petroli kwa muda mrefu sasa ambapo leo vituo vyote sita vya mfuta wilayani humo vimeishiwa petroli na kusababisha watumiaji kunua petroli kwa wauzaji  wa mitaani kwa shilingi elfu tano kwa lita.

Wakizungumza na ITV wamesema tatizo la kuadimika kwa mafuta imekuwa changamoto kubwa kwao na hivyo wameiomba serikali kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo.

kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mbinga Bw. Cosmas Nshenye amekiri kuwepo changamoto ya petroli na amesema inashughulikiwa na serikali.