Back to top

Wizara ya afya nchini Kenya imethibitisha maambukizi mapya 14 .

08 May 2020
Share

Wizara ya afya nchini Kenya imethibitisha maambukizi mapya 14 ya virusi vya Corona na kufanya idadi kufikia 621 .

Naibu waziri wa afya Dkt Rashid Aman anasema kuwa mtoto wa miezi 11 ni miongoni mwa watu 14 walioambukizwa wote wakiwa ni wakenya,visa vitatu vikiripotiwa Kaunti ya Mombasa Nairobi visa 10 na Machakos kisa kimoja.

Watu 13 wakiwa ni waliopatikana kwenye jamii baada ya zoezi la upimaji huku mtu mmoja akiwa karantini.

Kenya ikielezea hofu ya kusambaa zaidi kwa virusi vya Corona baada ya watu kuanza kutoroka mitaa ya Eastleigh na OLD Town huko Mombasa.

Wizara ya afya aidha inasema kuwa watu wengine watano wamepona na kufikisha 202 waliopona kufikia sasa.

Wahudumu 34 wa kiafya wakiwa miongoni mwa watu 621 ambao wameambukizwa virusi vya Corona Corona nchini kenya.

Serikali ikidokeza kuwa wakenya wanaoishi katika kambi za muda kufuatia mafuriko wataanza kuhamasishwa kuhusu jinsi ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Wizara ya afya pia imethibitisha kurejeshwa nyumbani kwa wakenya 237 waliokuwa wamekwenda nchini India kutafuta matibabu kabla ya kufutiliwa mbali safari za ndege kuingia na kutoka kenya.

Wote hao watawekwa karantini kwa siku 14 zijazo.