Back to top

Wizara ya madini yaagiza GGM kutekeleza maagizo ya serikali.

01 July 2020
Share

Siku chache baada ya waziri wa nishati kukataa ombi la mgodi wa GGM la kupewa miezi kumi na nane kujenga kituo cha kupokea umeme wizara ya madini imeunga mkono kauli hiyo huku ikiuagiza mgodi huo kutekeleza maagizo ya serikali.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mgodi huo Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko amesema serikali haitakuwa tayari kutoa kibali kutoka kwa wataalamu kutoka nje nchi kuja kujenga kituo cha umeme wakati nchi inawataalamu wa kutosha. 

Makamu wa raisi wa mgodi wa GGM Saimoni Shayo anasema mgodi huo uliomba wataalamu kutoka nje ya nchi ili kuhakikisha wanajenga kituo imara ambacho kitahimili na kulinda miundombinu ya uzalishaji dhahabu.

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel anasema wataalamu wa ndani wakipewa nafasi wanaweza badala ya kusubiri wataalamu kutoka nje kwa miezi kumi na nane.