Back to top

Wizara ya Madini yatakiwa kuthibiti utoroshwaji madini nje ya nchi.

27 September 2020
Share

Serikali imeitaka Wizara ya Madini kuongeza nguvu zaidi katika kudhibiti wizi na utoroshwaji wa madini nje ya nchi ili nchi iweze kunufaika na madini yanayochimbwa nchini.

Akifunga maonesho ya kimataifa ya teknolojia ya sekta ya madini mkoani Geita kwa niaba ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki amesema udhibiti ukifanyika vema basi taifa litanufaika zaidi na rasilimali zake.

Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko amewaonya wafanyabishara wanaouza madini feki hali inayoharibu sifa ya Tanzania kimataifa.