Back to top

Wizara ya Maliasili yaunda kikosi kazi cha kupambana na upotoshaji.

13 May 2020
Share

Wizara  ya Maliasili na Utalii imeunda kikosi kazi kitakachoshirikiana na taasisi zingine kukabiliana na watu wanaotoa taarifa za upotosashaji wa hatua zinazochukuliwa na serikali kukabiliana na tatizo la Corona.

 Akizungumza na wadau wa utalii jijini Arusha Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangala amesema pamoja na kikosikazi hicho pia kufanya mambo mbalimbali yanayolenga kufufua  biashara ya utalii ambayo inaendelea licha ya kuathirika na tatizo la Corona pia inaathiriwa na taarifa za upotoshaji zinazotolewa.

 Amesema hatua hizo ni sehemu ya matokeo ya kikao maalumu cha wadau wa sekta hiyo kilichofanyika kwa siku mbili jijini Arusha  kilicholenga kuendelea kuhakikisha utalii unafanyika sambambana tahadhari za kukababiliana na tatizo la Corona.


Amesema Pia wametengeneza mwongozo wa kuendesha shughuli za utalii utakaoelekeza namna ya wadau wanavyoweza kuishi na kuendeleza utalii pamoja na CORONA na pia kuandaa miongozo ukiwemo wa kuwa na Bima kwa watalii,kuwa na Bei zenye kuvutia utalii,hasa wakati huu ambao wengi walishafuta safari zao.