Back to top

Zaidi ya Milioni 175 walizotapeliwa walimu zaokolewa na TAKUKURU.

13 June 2020
Share

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Rukwa imeokoa zaidi ya shilingi millioni mia moja sabini na tano ambazo chama cha msingi cha ushirika cha Uwami kiliwatapeli walimu wastaafu.

Aidha, imezirejesha shilingi  milioni hamsini na sita, laki saba kati ya hizo kwa  walimu thelathini na tisa waliotapeliwa na chama cha ushirika cha msingi cha Uwami.

Akikabidhi fedha hizo kwa walimu hao walimu wastafu hao, Mkuu wa TAKUKURU mkoani Rukwa Bwana Hamza Mwenda shilingi milioni arobaini na tano, laki tatu na kumi na tano kati ya hizo zitareshwa katika akaunti maalm ya Benki Kuu ya Tanzania na shilingi milioni hamsini na sita na laki saba zitareshwa kwa walimu wote wastaafu waliotapeliwa na chama hicho.

Akiongea na walimu wastaafu waliotapeliwa fedha hizo, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bwana Joachim Wangavo amewahakikishia walimu hao juu ya usalama wa fedha zao.

Baadhi ya walimu wastaafu hao waliozungumza na ITV wameipongeza na kuishukuru serikali kupitia TAKUKURU kwa jitihada zilizowezesha kurejeshewa fedha zao.