Back to top

Zaidi ya watu 600 wamefariki tangu kuingia kwa kipindupindu nchini.

09 August 2018
Share

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto kwa kushirikiana Wizara ya Maji na umwagiliaji pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI wameanza mikakati ya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao tangu uingie nchini umeshasababisha vifo vya watu zaidi ya 600 huku wengine elfu thelathini na mbili wakiuugua ugonjwa huo.

Akizungumza na wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwemo Shirika la Afya duniani WHO Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema wizara hiyo pekee haiwezi kutokomeza ugonjwa huo bila kushirikiana na wadau wengine ili kuweka mbinu za kukabiliana nazo.

Kwa upande wake Afisa Udhibiti wa magonjwa na majanga kutoka Shirika la Afya duniani WHO nchini Tanzania Dkt Grace Saguti amesema itakapofika tarehe 15 Agosti mwaka huu Tanzania itakuwa imetimiza miaka mitatu tangu ugonjwa huo uliporipotiwa ambapo amesema endapo miundombinu ya maji itaimarishwa kutawezesha kukabiliana na ugonjwa huo.