Back to top

Zoezi la uokoaji linaendelea Lebanon.

07 August 2020
Share

Zoezi la uokoaji bado linaendelea nchini Lebanon la kuitafuta miili ya watu waliofukiwa kwenye kifusi katika bandari ya Beirut baada ya kutokea mlipuko mkubwa siku tatu zilizopita ambapo kwa mujibu wa Serikali ya Lebanon miili mingine mitatu imepatikana katika muda wa saa 24 zilizopita.

Maafisa wa uokoaji kutoka Ufaransa na Urusi wakisaidiwa na mbwa maalumu wanaendelea na zoezi la kuitafuta miili ya watu pamoja na uchunguzi katika eno la bandari mjini Beirut.

Rais wa Lebanon Michel Aoun anasema tani 2,750 za kemikali ya ammonium nitrate zilikuwa zimehifadhiwa kwa njia isio salama katika ghala moja na kusababisha mlipuko.