
Watu wengine tisa wakiwemo saba wa familia moja , mhudumu wa afya na mke wake, wamekutwa na virusi vya Ebola, katika hospitali ya rufaa ya taifa nchini Uganda ya Mulago.
Hofu imeendelea kuongezeka kwamba mlipuko huo huenda usiweze kudhibitika, huku idadi ya maambukizi ikiendelea kuripotiwa katika mji mkuu.
