Back to top

Wenye verification Tweeter kuanza kulipia $20

31 October 2022
Share

Mmiliki mpya wa mtandao wa Tweeter Elon Musk amewaagiza wafanyakazi wa mtandao huo kuhakikisha kuwa hadi ifikapo Novemba 7, 2022 wawe wamepandisha gharama ya watumiaji wanaolipia mtandao huo kupitia kipengele cha Twitter Blue kutoka Dola $4.99 hadi Dola $19.99 kwa mwezi ambapo amebainisha kuwa mabadiliko hayo yatahusu pia akaunti zilizothibishwa (Verified Accounts) huku akiongeza kuwa wafanyakazi wanaoshughulikia mabadiliko hayo watafutwa kazi endapo hayatazinduliwa ifikapo Novemba 7.
.
Hata hivyo, akaunti ambazo tayari zimethibitishwa zitapewa siku 90 za kujisajili kwenye Twitter Blue, ikiwa akaunti hizo hazitafanya hivyo zitapoteza beji zao.