Back to top

UTURUKI NA URUSI KUTETA ILI KUREJESHA MKATABA USAFIRISHAJI NAFAKA

02 November 2022
Share

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, atazungumza na Rais wa Urusi Vladimir Putin na wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika siku zijazo kwa lengo la kurejesha mkataba wa usafirishaji wa nafaka.

Hayo yamesemwa na aziri wa mambo ya nje ya Uturuki Mevlut Cavusoglu wakati alipozungumza na waandishi habari mjini Istanbul.


Cavusoglu amesema wanaamini watafanikiwa kupata muafaka kwa kuwa mkataba huo una manufaa kwa kila mtu.

Urusi ilitangaza Jumamosi iliyopita kuwa inasitisha ushiriki wake katika mkataba huo uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki mwezi Julai ambao uliruhusu usafirishaji wa nafaka ya Ukraine kuanza tena.