
Mkuu wa TAKUKURU mkoani Kagera, John Joseph amesema Taasisi hiyo inawashikilia watu watano ambao ni mawakala wa kusajili laini za simu za mikononi, kwa tuhuma za kusajili laini za ziada kwa kutumia vitambulisho vya NIDA vya wateja wanaokwenda kusajili laini kwa mawakala hao, kisha kuzisambaza laini hizo kwa wanaotumia mitandao kuwatapeli wananchi, huku akibainisha kuwa wanaendelea na uchunguzi, utakapokamilika watawafikisha watu hao mahakamani.
