Back to top

Polisi wadaiwa kupokea Rushwa kwa wafugaji, Lindi

02 November 2022
Share

Wananchi wa Kata ya Kibutuka iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, wamedai kuna baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi wanaopokea rushwa kutoka kwa wafugaji,  waonapofanya makosa ili wasichukuliwe hatua za kisheria.
.
Wananchi hao wametoa malalamiko hayo kwa Kamishna wa Oparesheni ya Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi, CP Awadhi Haji, ambapo amewataka wananchi hao kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo ,ili kuwatambua askari wanaopokea rushwa ili wawajibishwe.