Back to top

BAADA YA SHAMBULIO, IMRAN KHAN YU BUHERI WA AFYA

04 November 2022
Share

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan, ameripotiwa kuwa katika hali nzuri, baada ya kupigwa risasi mguuni katika mkutano wa kisiasa kwa kile rais wa taifa hilo Arif Alvi, alichosema ni jaribio la kumuua.

Kulingana na Afisa wake wa karibu, Raoof Hasan, waliotekeleza tukio hilo walitaka kumuua Khan, huku akithibitisha kuwa mshambuliaji wa kwanza ameuwawa kwa kupigwa risasi na mwingine amekamatwa.

Khan amekuwa akiongoza maandamano tangu siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita kutoka mji wa Lahore, kuelekea mji mkuu Islamabad, akitaka kufanyika kwa uchaguzi mpya baada ya kuondolewa madarakani mwezi Aprili.