Back to top

ISRAEL:MAPIGANO NA HAMAS YAANZA TENA.

01 December 2023
Share

Jeshi la Israel limesema sasa limeanza tena mapigano na Hamas mjini Gaza ambapo Israel imeanza tena kulipua Gaza baada ya kumalizika kwa muda wa makubaliano.

Katika chapisho kwenye X, Vikosi vya Ulinzi vya Israeli vilisema kuwa Hamas walifyatua risasi dhidi ya Israel, na hivyo kukiuka masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano.

Awali Israel ilisema ilizuia roketi iliyorushwa kutoka Gaza huku vyombo vya habari vinavyoshirikiana na kundi la Hamas vikiripoti milipuko na milio ya risasi Kaskazini mwa Gaza.

Makubaliano ya kusitisha mapigano hayo yalipangwa kudumu kwa siku nne lakini muda uliongezwa mara mbili.

Hadi kufikia Alhamisi, mateka 110 waliokuwa wameshikiliwa huko Gaza wameachiwa huru tangu kuanza kwa mapatano hayo tarehe 24 Novemba, huku Israel ikiwa imewaachia huru wafungwa 240 wa Kipalestina.