Back to top

BIL. 66 KUREJESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA ILIYOHARIBIKA

25 April 2024
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametoa Bilioni 66, kwa ajili ya kuanza urejeshaji wa miundombinu ya barabara zilizoharibika nchini.

Fedha hizo tayari zimegawanywa kwa Mameneja wa TANROADS mikoa yote iliyoathirika, kwa ajili ya kufanya kazi kwa haraka usiku na mchana ili kurekebisha kadhia zilizozikumbumba barabara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
 
Akizungumza Jijini Arusha mara baada ya kukagua Barabara ya Afrika Mashariki (Arusha bypass) iliyoharibiwa na mvua hizo, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Mohamed Besta, amesema kuwa kutokana na udharula huo tayari Rais Samia ametoa fedha za matengenezo ya miundiombinu hiyo ambazo zimeshapelekwa katika Mikoa yote Nchini.

Mhandisi Besta amesema kuwa tayari kazi inaendelea katika maeneo yote nchini na fedha hizo zinaratibiwa na vitengo maalumu vya dharula vilivyopo TANROADS pamoja na ofisi za mikoa.