Back to top

JELA MAISHA, KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 8

25 April 2024
Share

Hamadi Tofki mwenye umri wa miaka 28, mkazi wa Kimambila, Kata ya Lubungo wilayani Mvomero, mkoani Morogoro amehukumiwa kifungo cha maisha jela, kwa kosa la kubaka mtoto wa miaka 8.
.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mvomero, Anthony Ngowi, amesema kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 25, 2023, huko Kimambila, Kata Lubungo, wilayani Mvomero kwa nyakati tofauti, ambapo mtuhumiwa alikuwa akivizia kipindi wazazi hawapo nyumbani na kwenda kumbaka mtoto huyo.
.
Baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi na ushahidi kukamilika mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani na kukutwa na hatia.