Back to top

WAZIRI SILAA ATAKA MAAGIZO YA MHE.RAIS YATEKELEZWE, TANGA

25 April 2024
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa, amewataka wananchi wa Kijiji cha Mianga kilichopo katika Tarafa ya Bwembela, Wilaya Muheza mkoani Tanga, kuzingatia maagizo yaliyotolewa na Rais Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, kuhusu mipango ya matumizi bora ya ardhi ya Kijiji hicho.

Waziri Silaa amesema hayo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijijini hapo kwa ajili ya kusikiliza mgogoro wa wananchi hao na serikali juu ya mashamba sita ya Azimio kilakula, Kibaranga, Bwembela Estate, Kihukwi, Sagiusi na Lewa.

Katika maagizo hayo Mhe.Rais aliagiza kufanyika upimaji wa mashamba hayo pamoja na kugawa ekari mbili mbili kwa kila mwanachi.

Mashamba hayo yalifutiwa hati mwaka 2016 na kuwa chini ya Serikali kwa usimamizi wa halmashauri ya Wilaya ya Muheza.