Bei ya Saruji Kalambo mkoani Rukwa Pasua kichwa.

Wananchi wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamelalamikia kupanda kwa bei ya saruji kutoka shilingi elfu kumi na sita hadi kufikia shilingi elfu ishirini na moja kwa mfuko wa kilo hamsini.

Kutokana na hali hiyo wananchi hao wameiomba serikali kuingilia kati suala hilo kutokana na kushindwa kumudu gharama hizo kutokana na hali halisi ya maisha.