Milipuko na milio ya risasi yasikika Nairobi,Kenya.

 

Milipuko na milio ya risasi imesikika katika eneo la 14 Riverside, Nairobi ilipo hoteli ya kifahari ya DusitD2 .

Msemaji wa kundi la kigaidi la al-Shabab ameliambia shirika la habari la BBC kuwa kundi hilo ndiyo limehusika katika tukio hilo.

Wataalamu wa kutegua mabomu wawasili eneo la tukio ambapo watu kadhaa wanasadikiwa kupoteza maisha.