Independent Television Ltd
Wanachama zaidi ya 400 wa Simba waenda bungeni wakitaka Rage awajibishwe.

 Zaidi ya wanachama 400 kutoka matawi mbalimbali ya klabu ya simba wamefunga safari kutoka jijini dar es salaa mmpaka bungeni mjini dodoma wakimtaka spika wa bunge anne makinda amfikishe kwenye kamati ya maadili ya bunge mwenyekiti wa klabu hiyo ismail aden rage ambaye pia ni mbunge jimbo la tabora mjini kwa madai ya kukiuka katiba ya simba na kuendesha klabu hiyo kibabe kinyume na sheria za nchi zinavyoelekeza.

ITV ilifika nje ya viwanja vya bunge na kushuhudia baadhi ya wanachama waliowawakilisha wenzao wakipiga kambi nje ya bunge kumsubiri spika wa bunge ili kufikisha kilio chao ambapo wamesema wamechoshwa na kile wanachodai mwenyekiti wa Simba Ismail Rage kuisigina katiba ya klabu hiyo kwa maslahi yake binafsi ilhali akijua klabu hiyo imesajiliwa kwa mujibu wa sheria za nchi ambazo hutungwa na chombo hicho cha kutunga sheria cha bunge.

Hata hivyo wanachama hao hawakufanikiwa kufikisha ujumbe wao kutokana na kutozingatia taratibu za bunge na kuahidi kurejea jijini Dar es Salaam kujipanga upya ambapo jitihada za ITV kumtafuta mwenyekiti Rage ili kuzungumzia hatua ya wanachama hao ziligonga mwamba kutokana na mbunge huyo kudaiwa kuwa safarini kikazi.

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather