Bunge limeitaka serikali izichukulie hatua taasisi zote za umma ikiwemo Wizara ya Malisili na Utalii kwa matumizi mabaya ya mabilioni ya fedha kinyume na utaratibu.
Wakichangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya (PAC ) iliyowasilishwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo hiyo baadhi ya wabunge wamesema fedha zilizotengwa kwa ajili ya Mradi wa Umeme Vijijini( REA) zaidi ya bilioni 1.8 zimetumika vibaya.
Aidha wabunge hao wamesema kitendo cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kutumia zaidi ya bilioni 10 kununua vifaa vingi ambavyo havihitajiki ni harufu ya rushwa.
Wabunge hao pia wamesema kuna haja ya baadhi ya taasisi za serikali zinazodaiwa gharama za umeme na Tanesco walipe ili liweze kujiendesha kiufanisi.