DC ataka wanafunzi wanaotembea km 20 kwenda shule kutafutiwa mabweni.

Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dkt. Halfani Haule amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Sumbawanga Jacobu Mtalitinya kuhakikisha anawahamishia kwenye hosteli wanafunzi wote wa kike wanaotembea umbali wa zaidi km 20 kutoka   Nambogo hadi Moro wakati wakienda Shule  ya Sekondari Kalangasa kwa lengo la kuwaepusha na vishawishi ambavyo vinaweza kusababisha kukatisha masomo  yao ikiwemo kupata ujauzito.