Back to top

KIMBUNGA 'HIDAYA' CHAPOTEA BAADA YA KUINGIA MAFIA

05 May 2024
Share

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imetangaza kuwa kimbunga “HIDAYA” kilichokuwa katika Bahari ya Hindi mashariki mwa Pwani ya nchi yetu, kimepoteza nguvu yake baada ya kuingia nchi kavu katika kisiwa cha Mafia.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo, ambayo inahitimisha mfululizo wa taarifa za kimbunga hicho, imeeleza kuwa hakuna tena tishio la kimbunga “HIDAYA” katika nchi yetu, licha ya uwepo wa mabaki ya mawingu ya mvua yaliyokuwa yakiambatana na kimbunga hicho ambayo yalisambaa katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa kusini mwa nchi yetu hususan katika maeneo ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Morogoro na maeneo jirani. 
.
Aidha Mamlaka hiyo imewashauri wananchi kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka kwenye Mamlaka hiyo pamoja na kufuata maelekezo na miongozo inayotolewa.