Naibu Waziri wa Fedha amezitaka Benki kushusha viwango vya riba.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezitaka Benki nchini kushusha viwango vya riba za mikopo ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi wakiwemo wakulima kunufaika na huduma za kifedha zinazotolewa na taasisi hizo za fedha kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua rasmi Benki ya Azania tawi la Sokoine na kusisitiza kuwa Benki zinanafasi kubwa wa kuisaidia nchi kufikia azma yake ya kuwa ya viwanda ifika mwaka 2025 kwa kukuza mitaji ya wananchi.