Wananchi wa kijiji cha Makame wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi

Wananchi wa kijiji cha Makame  kata ya Makame wilaya ya Kiteto mkoani Manyara wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi na salama hali inayowalazimu kutumia maji ya visima na mabwawa ambayo hutumiwa na mifugo hivyo kuhatarisha uasalma wa afya zao. 

Wakizungumza na ITV wananchi hao wameeleza adha wanazozipata kwa kukosa maji safi na salama na kuiomba serikali itatue changamoto hiyo.

Mjumbe wa serikali ya kijiji hicho amesema kuwa tatizo hilo limedumu kwa muda mrefu  hali ambayo inaweza kuathiri juhudi za wananchi kujiletea maendeleo iwapo watatumia maji yasiyo salama.

Meneja wa  mamalaka ya maji vijijini wilaya ya Kiteto (RUWASA) Mhandisi Stephano Mbarouk ameeleza mikakati ya serikali katika kutatua changamoto hiyo.