Watu watatu wafariki kwa kusombwa na Maji Tarime mkoani Mara.

Watu watatu wakazi wa wilaya ya Tarime mkoani Mara  wamefariki baada Kusombwa na maji wakati  wakukatiza daraja la Mto Msati  linalounganisha barabara ya kutoka Mwanza kwenda Sirari kukatika   kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani hapa.

Kamanda wa Polisi  Kanda Maalumu ya Tarime Rorya William Mkonda akizungumza kwa njia ya simu  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.