Back to top

MVUA YALETA ATHARI JIMBO LA KAVUU MKOANI KATAVI

15 April 2024
Share

Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta athari katika jimbo la Kavuu ,lililopo katika Halmashauri ya Mpimbwe, wilaya ya Mlele ,mkoa wa Katavi, ambapo mvua hizo zimekata mawasiliano katika madaraja ya mto Msadya pamoja na daraja la Mto Kibaoni ,katika Halmashauri ya Mpimbwe.

Katika eneo la Mto Msadya umehama njia yake hadi maeneo ya makazi ya watu na kusababisha adha kwa magari na wananchi wanaotumia daraja hilo, hususani katika vitongoji vya Ikuba, Usenga na Igongo.

Upande wa  daraja la kibaoni, mawasiliano baina ya Kibaoni na Usevya katika Halmashauri hiyo ya Mpimbwe yamekatika na kusababisha njia kufungwa kutokana na maji kuvunja daraja hilo.

Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mhe.Geophrey Pinda, akiwa na viongozi wa serikali na Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mlele, wamefika maeneo yaliyoathirika kwa lengo la kujionea uharibifu na athari iliyopapatikana kwa wananchi.

Mhe, Pinda amewapa pole wote walioathirika na mafuriko hayo huku akiwataka wananchi hususan vijana wanaoishi eneo la mto Msadya kuanza kuchukua hatua za uhifadhi maingira.